Miongozo

Kila kitu unachohitaji kujua ili kutumia DUKAIO kama mtaalam.

Utangulizi

Karibu kwenye DUKAIO, mfumo wako wa kisasa wa kusimamia mauzo na stoo. Mwongozo huu utakusaidia kuelewa kila hatua ya kutumia mfumo huu ili uweze kukuza biashara yako kwa ufanisi.

Hatua ya Kwanza:

Sajili akaunti yako, ingia, anza kurekodi bidhaa na mauzo. Mwisho wa trial au kifurushi ku-expire, utatumia ukurasa wa Renew kutuma ushahidi wa malipo.

Setup ya Mfumo

  1. Sajili akaunti mpya kwenye ukurasa wa Login -> Sajili Akaunti.
  2. Weka jina la duka, username, simu, na password imara.
  3. Baada ya kuingia, nenda Settings kuweka taarifa za biashara (logo, n.k).
  4. Weka bidhaa zako kwenye Products kabla ya kuanza kuuza.

Kuelewa Dashboard

Dashboard ndio kitovu cha biashara yako. Hapa utaona takwimu Muhimu kwa muhtasari:

Usimamizi wa Stoo (Stock)

Kusimamia bidhaa ni rahisi. Fuata hatua hizi:

1. Ongeza Bidhaa

Nenda kwenye tab ya 'Products', bonyeza 'Add Product', weka jina, bei ya kununua, bei ya kuuza, na idadi.

2. Badili Stock

Unaweza kuongeza stock mpya inapofika dukani kwa kutumia kitufe cha edit kwenye bidhaa husika.

Kufanya Mauzo (POS)

Mfumo wa POS umetengenezwa kuwa wa haraka zaidi:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa 'Sales'.
  2. Tafuta bidhaa kwa kuandika jina lake.
  3. Chagua idadi (quantity) ya bidhaa mteja anayochukua.
  4. Bonyeza 'Kamilisha Mauzo'.
  5. Mfumo utapunguza stock ya bidhaa hiyo moja kwa moja.

Risiti (Receipts)

Ripoti na Uchambuzi

Pata ufahamu wa kina wa faida unayotengeneza:

Ukurasa wa 'Reports' unakuonyesha faida halisi (Gross Profit) kwa kutoa gharama ya manunuzi kwenye mapato ya mauzo. Unaweza kuchuja ripoti kwa siku, wiki, mwezi, au mwaka.

Kulipia na Kuhuisha (Renewals)

Kama kifurushi chako kimekwisha muda wake, utapelekwa kwenye ukurasa wa 'Renew'.

Chagua mpango mpya, fanya malipo kupitia namba zinazoonyeshwa, na pakia picha ya muamala (screenshot). Mara tu baada ya admin kuhakiki, uwezo wa kutumia mfumo utarejea.

Admin: Uhakiki, Notifications, Backup

Tatizo la Kawaida & Suluhisho

Bado una maswali? Tuko hapa kwa ajili yako.

Wasiliana na Huduma kwa Wateja